Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Mustafa Bairam, waziri wa zamani wa Lebanon, katika hafla iliyoandaliwa kutokana na mnasaba wa maadhimisho ya pili ya shahada ya shahidi mpiganaji, Hassan Moussa Diqa, maarufu kwa jina la “Usama”, iliyofanyika katika Husseiniyya ya kijiji cha Hazin, alisisitiza kuwa muqawama nchini Lebanon, pamoja na watu wake, umeweza kutekeleza viwango vya juu kabisa vya wajibu wa kibinadamu na kitaifa katika kusimama pamoja na waliodhulumiwa, licha ya wingi wa wanaosuluhisha na wanaopanga njama.
Katika hafla hiyo, Abbas Mazlum, msimamizi wa sekta ya nane ndani ya Hizbullah, pamoja na wanaharakati wa manispaa, wa maeneo ya ndani, ya kijamii, ya kitamaduni, wanazuoni wa dini, familia za mashahidi na kundi la wakazi walihudhuria.
Alisisitiza kuwa kile ambacho Lebanon inafaidi leo katika suala la mamlaka na heshima ni matunda ya kujitolea kwa muqawama na damu za mashahidi.
Bairam, akieleza kwamba muqawama si burudani wala si chaguo la bahati nasibu (la muda), bali ni utamaduni wa maisha na njia ya heshima na utu, alisisitiza kuwa; kama muqawama usingekuwapo, Lebanon isingekuwa na uzito wala hadhi yoyote.
Aliongeza kuwa; adui licha ya mauaji, uharibifu na machinjio aliyoyatekeleza katika siku za mwanzo za vita, hakuweza kuvunja azma ya muqawama; muqawama huu uliendelea kubaki thabiti na wenye nguvu, na ukaongeza uimara na uthabiti wake.
Waziri huyo wa zamani, akisisitiza kuwa harakati za muqawama zinajengwa juu ya uelewa, nguvu na uwajibikaji, si juu ya pupa wala uzembe, alitangaza kwa msimamo mkali kuwa: kujisalimisha hakuna nafasi katika kamusi ya muqawama.
Alibainisha kuwa; muqawama uko tayari kushirikiana na serikali ya Lebanon katika kulinda mamlaka ya nchi na kuwarejesha mateka, na akasema kuwa kuja kwa wajumbe nchini Lebanon ni dalili ya nguvu ya muqawama na nafasi yake yenye athari.
Hafla ilianza kwa usomaji wa aya za Qur’ani Tukufu, kisha ikaoneshwa filamu ya maandishi (makala ya kihistoria) kuhusu maisha na safari ya jihadi ya shahidi. Baadaye, watoto wa shahidi walimkabidhi waziri wa zamani Bairam cheti cha shukrani. Hafla ilihitimishwa kwa majlisi ya maombolezo ya Husseini iliyoongozwa na Sheikh Basim Farhat.
Maoni yako